Makamu wa Pili Mhe Hemed afungua Maabara

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla amesema shabaha kubwa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuwapatia huduma Bora wananchi wake pamoja na kuhakikisha huduma za Afya zinaboreshwa. Akiyasema hayo huko Binguni Wilaya ya Kati Unguja wakati wa ufunguzi wa Jengo la Maabara ya Utafiti na Upimaji wa Virusi vya uviko 19 pamoja na maradhi mbali mbali ya mripuko ikiwa ni moja ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi na mafanikio ya miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar Alisema katika kuimarisha huduma za afya ikiwemo kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Afya pamoja na kuwatatulia changamoto zao . Amewataka watumishi hao kuzitumia mashine hizo kwa umakini na uangalifu mkubwa kutokana na gharama kubwa ya vifaa hivyo Aidha aliwafahamisha wanasayansi chipukizi kuitumia taasisi ya utafiti ili kukuza vipaji vyao kwa manufaa yao na Taifa kiujumla Makamu huyo akitoa shukrani kwa Taasisi za utafiti za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,ikiwemo Taasisi ya utafiti na Magonjwa ya Binaadamu (National Institute of Medical Research -NIMR,) na Taasisi ya Afya ya Ifakara ,(Ifakara Health Institute -IHI ) .kwa mashirikiano makubwa waliyoyaonyesha pamoja na washiriki wa Maendelea kutoka Swiss Development Corporation na Shirika la Afya Ulimwengu Afisi ya Tanzania. Nae Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.Nassor Ahmed Mazrui amesema licha ya mafanikio mazuri yaliyopatikana lakini pia kunachangamoto mbali mbali ambazo zinahitaji kupatiwa ufumbuzi ikiwemo uhaba wa Fedha za kukamilishia majengo ya maabara ya biology na chemistry pamoja na rasilimali fedha za kuchunguzia tafiti muhimu. Kwa upande Afisa Muendeshaji Mkuu wa Taasisi ya Ifakara Bw.Martin Mfikiwa ameridhishwa na mashirikiano na Wizara ya Afya kuhakikisha lengo lilikusudiwa linafanikiwa kwa ufanisi mkubwa. Alieleza kuwa baadhi ya watumishi 17 wameshapatiwa mafunzo kwa vitendo ya matumizi ya mashine za kuchunguzia maradhi mbali mbali ikiwemo uviko 19.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *